SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: YANGA YAANZA NA USHINDI KWENYE MBIO ZA KUTETEA KOMBE LA FA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
RAUNDI ya tano ya mashindano ya FA [Azam Sports Federatio Cup] imeendelea leo uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo Ashanti Un...
IMG-20170121-WA0029


RAUNDI ya tano ya mashindano ya FA [Azam Sports Federatio Cup] imeendelea leo uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo Ashanti United walikuwa na kibarua kizito cha kuwakabili mabingwa watetezi wa kombe hilo, timu ya Yanga.

Licha ya kucheza mpira wa wazi bado haikuwa rahisi kwa Ashanti United ambao mpaka filimbi ya mwamuzi inapulizwa kuashiria mwisho wa mchezo, Yanga walikuwa na 4 wakati Ashanti wakipachika bao 1 pekee.

Goli la kwanza la Yanga   lilifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Amis Tambwe ambaye aliunganisha pasi iliyopigwa toka upande wa kulia na Msuva.
Dakika 37 Yanga walipata bao la pili kupitia kwa Thaban Kamusoko baada kuachia shuti kali nje ya kumi na nane lilomshinda mlinga lango wa Ashanti, Rajabu Kahumbu.
Msuva alifunga bao la tatu dakika ya 53 kwa penati baada ya Seleman Sultan kumchezea vibaya Msuva na muamuzi Ahmad Kikumbo kuamuru penati ipigwe na winga huyo akaweka mpira kambani.
Goli pekee la Ashanti lilifungwa dakika 61 na Isack Hassan ambaye aliwazidi ujanja mabeki wa Yanga.
Yusuph Muhilu alikamilisha karamu ya magoli dakika ya 89 baada ya kufunga bao la nne kwa kumalizia krosi ya Emmanuel Martin toka upande wa kushoto.
Kesho kutakuwa na mchezo mwingine katika michuano hii kati ya Simba na Polisi Dar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top