Je, wamjua Zlatan Ibrahimovic?

Hakuna kitu kingine
ambacho kimekuwa kikituunganisha walimwengu wote kama mchezo wa soka na bila
kujijua tumekuwa tunawafaham watu wengi ambao pengine ni nadra sana kukutana
nao uso kwa uso.
Pamoja na Sanaa nyingine kadha
wa kadha ikiwemo miziki, siasa, michezo mbalimbali ya kuigiza, mpira wa kikapu,
masumbwi itupelekeayo kuwafahamu watu mbalimbali wa kimataifa, mchezo wa mpira
wa miguu umetuunganisha na ulimwengu mzima na kujihisi sasa kama tupo wote
sehemu moja na pengine kujihisi hata tunaweza kuwa tukipiga stori kwa ukaribu Zaidi kumbe la, hasha.
Ukikaa kwenye vikundi vya
watu mbalimbali, mkawa mnapiga soga za hapa na pale za kimichezo, mkawa
mnawatafuta wanadinga walioonyesha vipaji vya hali ya juu, wakati unawataja
akina Diego Almando Maradona, Emmanuel Pettit, TIELY Henry, Luis Figo, Yohan
clayff pamoja na akina Zinedine Zidane wa kizazi hicho, lakini pia ukawakumbuka
akina Lionel Messi, Adjen Robben, Christian Ronaldo, hakika ni makosa sana
kumsahau Zlatan Ibrahimovic akifahamika kwa jina la Ibra Kadabla.
Zlatan Ibrahimovic mwenye
umri wa miaka 34 na urefu wa mita 1.95 akicheza kama mshambuliaji namba 9 alizaliwa
mnamo tarehe 3 ya mwezi wa kumi mwaka 1981, Malmo, huko nchini Sweden.
Akiwa anatarajiwa
kuihudumu klabu ya Manchester united msimu ujao baada ya kusajiliwa kwa
uhamisho huru kutoka klabu ya PSG, Kadabla kariya yake ya soka alianza katika
timu ya malmo akiwa na timu ya vijana na kufanya vyema sana na kupandishwa
katika timu ya wakubwa mwaka 1999.
Aliweza kuitumikia Malmo
kwa miaka miwili kabla ya kufanya uhamisho kwenda klabu ya nchini uholanzi timu
ya Ajax ambapo hapo alidumu kwa miaka mitatu. Mwaka 2004 alisajiliwa na timu ya
Juve ya nchini Italy kwa uhamisho wa Euro 16m. Napo hapo hakudumu pia na kusajiliwa
na klabu ya Inter kwa gharama ya euro 24.8mil.
Bado safari ya kadabla
ilikuwa inaendelea. Pamoja na kufanya makubwa akiwa na Inter, bado alikuwa na
hamu ya kuendelea kupata changamoto nyingine kutoka vilabu tofauti na katika
mwaka wa 2009 alisajiliwa na klabu ya FC Barcelona kwa uhamisho ghari Zaidi wa
Euro 68.50mil na akiwa klabuni hapo alifanikiwa kutwaa kombe la ligi ya
mabingwa barani ulaya huku wakichukua na kombe la ligi ya Hispania. Napo
Barcelona hakudumu sana na hivyo kusajiliwa na AC Milan kwa mkopo. Mwaka 2011
uhamisho wa mkopo wa Kadabla ukakomea hapo na AC Milan wakamchukua tena kwa
usajili wa Euro 24milna kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa Zaidi duniani.
Mwaka 2012 klabu ya
nchini Ufaransa PSG wakavutiwa na namna ya uchezaji wa Kadabala na kumsajili
kwa ada ya juma ya Euro 22mil na kufanya makubwa akiwa na PSG kama kuchukua
kombe la legie 1 mara 3 na kombe la Ufaransa mara 2 huku akifunga magoli 162
akiwa na klabu ya PSG.
Mwaka huu kandarasi yake
ilikuwa imefika kikomo na hivyo kuondoka klabuni hapo na kusajiliwa na timu ya
Manchester United ambayo imepoteza mvuto tangu kuondoka kwa aliyekuwa mkufunzi
wa klabu hiyo kwa muda hivi Sir Alex Fergason na sasa iko chini ya Jose Morinho
akitegemewa kuirudisha klabu hiyo katika
enzi zake za zamani. Uwezo wa Zlatan Ibrahimovic sina shaka nao, laikini shaka
yangu ni uhitaji wa United mafanikio ya haraka ambao kwangu naona laweza kuwa
tatizo kwani huenda akatamani kufanya vingi, lakini umri unamvuta mkono na
kumrudisha nyuma na kuwafanya mabosi wa klabu hiyo kumtimulia mbali.
Mechi yake ya kwanza timu
ya taifa ya Sweden ilikuwa ni 2001 nakuendelea kuihudumu timu hiyo bila
mafanikio huku 2010 akiteuliwa kuwa nahodha mpaka anatundika daruga baada ya
umri wake kumtupa mkono. Akiwa timu ya taifa, Kadabla alifanikiwa kuifungia
timu hiyo magoli 62.
Huyo ni Zlatani
Ibrahimovic anayetegemewa kuirudisha hadhi ya klabu ya Manchester United wakati
huku umri unamtupa mkono. Japo anaweza kuonyesha mchango mkubwa lakini
changamoto za vijana wenye damu change wanaotafuta jina kama akima Rashford
kwake inaweza kuwa kikwazo huku changamoto ya kukutana na ugumu wa ligi ya
wingereza. Kila la kheri Kadabla ukifahamu ya kuwa ile sio legie 1 tena,
utakutana na akina Sauthomptom, everton Liverpool na vilabu vikubwa vinavyoweza
kuumaliza uwezo wa miguu yako.
Post a Comment