Wachezaji wa zamani wa Manchester united waibeba ureno.

Na Charles Kunji
Timu ya taifa ya Wales imekubali kichapo cha goli 2-0 dhidi
ya timu ya taifa ya ureno katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza wa kombe la
euro linalofanyika huko nchini ufaransa.
Goli la kwanza la timu ya taifa ya ureno, lilifungwa na
nahodha wa timu hiyo, mshambuliaji wa kimataifa anayekipiga katika timu ya Real
Madrid C. Ronaldo, dakika ya 50 akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Rafael
Guameiro wakati goli la pili likifungwa na Lous Nani dakika ya 53 akimalizia
pasi murua ya Ronaldo.
Wafungaji wa magoli wote walishawahi kukipiga katika klabu ya
Manchester United kwa mafanikio kadhaa na baadae wote wakatimkia mahala pengine
kwa ajili ya kutafuta maisha mengine ya mpira. Wakati Ronaldo akiendelea kukihudumu
kikosi cha Real Madrid, Nani yeye amesaini mkataba wa miaka mine kuihudumu
klabu ya Hispania, timu ya Valencia.
Pamoja na Wales kutumia mbinu tofauti, huku wakimtegemea
mchezaji wao tegemezi Gareth Bale aliyekuwa akihaha uwanja mzima kujaribu kuibeba
Wales, bado haikusaidia kitu mbele ya nyuso za akina Renato Sanchezi, Nani
Ronaldo na wengineo waliokuwa na nia ya kuhakikisha wanaipeleka timu yao hatua
ya fainali.
Ronaldo amewafikia akina Payet, Bale, Giroud wote wakiwa na
magoli matatu huku Antonio Greezman akiongoza kwa jumla ya magoli manne.
Lakini pia ni kitu kizuri kwa ronaldo goli la kichwa alilofunga limefikia idadi ya magoli 9 rekodi aliyokuwa anaishikia mchezaji wa zamani Michel Plattin na kumpa hamasa endapo atapata goli katika mchezo wa fainali utamfanya kuivunja rekodi hoyo na kuweka rekodi yake.
Lakini pia ni kitu kizuri kwa ronaldo goli la kichwa alilofunga limefikia idadi ya magoli 9 rekodi aliyokuwa anaishikia mchezaji wa zamani Michel Plattin na kumpa hamasa endapo atapata goli katika mchezo wa fainali utamfanya kuivunja rekodi hoyo na kuweka rekodi yake.
Kwa timu ya Wales, haya ni mafanikio makubwa kwao kwani tangu
mwaka 1958 walikuwa hawajafuzu matika mashindano yeyote makubwa na kufuzu kwao
euro mwaka huu mpaka kutolewa hatua ya nusu fainali ni mafanikio makubwa kwao
na kuweka rekodi nyingine.

Wales itawasubiri kati ya timu ya ufaransa au ujerumani
itakayofungwa kwa ajili ya kutafuta mshindi wa tatu kabla ya kupisha fainali ya
kumtafuta bingwa wa ulaya.
Post a Comment