SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MESSI AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 21
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MESSI AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 21 Mchezaji wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela...

MESSI AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 21


Messi-Jela





Mchezaji wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa makosa ya ukwepaji kodi.
Baba yake pia amehukumiwa kifungo cha kwenda jela kwa makosa hayohayo ya udanganyifu wa Euro milioni 4.1 (paundi ml 3.5; dola ml 4.5) kati ya mwaka 2007 na 2009.
Hata hivyo, hakuna uwezekano wa mmoja kati ya wawili hao kutumikia kifungo chochote.
Kwa mujibu wa mfumo wa kisheria wa nchini Uhispania, kifungo cha chini ya miaka miwili kinachukuliwa kama onyo (unakuwa chini ya uangalizi maalum).
Jana Jumatano mahakama ya jijini Barcelona iliwatia hatiani Messi na baba yake kwa makosa ya ukwepaji kodi kwa miezi mitatu.
Messi amepigwa faini ya euro mil 2 na baba yake euro mil 1.5.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top