SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Huu ndio Ujumbe wa Schweinsteiger Kwa Mashabiki wake.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya mashetani wekundu, Bastian Schweinsteiger amesema kwamba bado ana furaha kuishi jijini Manchester licha...

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya mashetani wekundu, Bastian Schweinsteiger amesema kwamba bado ana furaha kuishi jijini Manchester licha ya kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo na kocha Jose Mourinho.
Mjerumani huyo ameondolewa na kuwekwa kwenye kikosi cha akiba na kocha Jose Mourinho, ambaye alithibitisha kwamba haihitaji tena huduma ya Schweinsteiger.
Schweinsteiger anatarajiwa kuondoka United mwishoni mwa dirisha hili la usajili na ametoa upadate nyingine kwa mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Twitter ametweet:
“Baada ya mizunguko yangu, nafurahia muda uliosalia katika siku ya leo hapa Manchester. Natumaini wote mna siku njema!”
United wanaonekana hawana mpango tena na Schweinsteiger na kaka yake Bastian, Tobi Schweinsteiger alinukuliwa akikosoa kitendo hicho alichofanyiwa mdogo wake na ku-tweet: “No respect.”
Mpaka sasa, United wanaviungo wa kati watano ambao ni Paul Pogba, Michael Carrick, Morgan Schneiderlin, Marouane Fellaini na Ander Herrera.
Ripoti zinaeleza kwamba, klabu za AC na Inter Milan zinahitaji huduma ya Schweinsteiger, ambaye atatakiwa kupunguza sana mshahara wake endapo ataamua kuondoka.
Anatajwa kupokea kiasi cha paundi 200,000 kwa wiki.
Msimu uliopita, Schweinsteiger alianza kwenye michezo 21 na michezo 10 aliingia kutokea benchi.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top