
Kuelekea kuanza kwa
msimu mpya wa ligi, wachambuzi wa soka katika kituo cha runinga cha Sky Sports
wametoa utabiri wao timu itakayotwaa ubingwa na zile zitakazomaliza katika
nafasi nne za juu.
Katika utabiri wao,
wachambuzi hao ambao ni Thierry Henry, Gary Neville na Jamie Carragher
wameiondoa kabisa Leicester katika kinyang’anyiro hicho.
Badala yake, wametupia
karata yao ya ubingwa kwa vilabu vya jiji la Manchester. Kitu ambacho kimsingi
si cha kushangaza, ukizingatia namna walivyofanya usajili wao kuanzia makocha
mpaka wachezaji.
THIERRY HENRY
1.
Man City 2. Man Utd. 3. Chelsea 4. Arsenal
“Siku zote matumaini
yangu yapo kwa Arsenal. Lakini nadhani ubingwa utachukuliwa na kati ya City au
United. Lakini kwasababu natakiwa kutaja timu moja basi naipa City.
“Chelsea hawatakuwa na
Michuano yoyote ya Ulaya, hivyo itakuwa faida kwao, lakini inaweza kuchukua
muda kidogo kuendana na kile anachowafundisha Conte.
“Vivyo hivyo kwa
Mourinho na Man Utd. Vilevile City na Guardiola- hivyo basi, labda kuna upenyo
kwa Liverpool, Arsenal na Tottenham – ambao wamekuwa na vikosi vyao vile vile
pamoja na makocha wale wale.”
GARY NEVILLE
1.
Man Utd 2. Arsenal 3. Man City 4. Liverpool
“United wana meneja na
wachezaji wawili ambao wana ari kubwa ya ushindi. Uwepo wa Jose Mourinho,
Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba – na wachezaji wengine ambao walikuwepo awali,
basi naiona United ikirejea kwenye uimara wake.
“Kuna wachezaji ambao
wanavaa tisheti za United na kuwaingia kwenye mioyo yao na kupambana kwa nguvu
– na hiyo sasa ndiyo Manchester United inavyopaswa kuwa.
“Kwangu mimi, bingwa
atakuwa Man Utd, Arsenal nafasi ya pili Arsenal, Manchester City nafasi ya tatu
na Liverpool nafasi ya nne.
JAMIE CARRAGHER
1.
Man City 2. Chelsea 3. Man Utd 4. Liverpool
“Kwa miaka mingi sana
nimekuwa nikisema kwamba City wana kikosi bora, lakini hawafanyi kile
kinachotakiwa na nadhani njaa ya mafanikio itarudi tena chini ya utawala wa Pep
Guardiola.
“Bila shaka,
wanahitaji kusajili zaidi, lakini tayari wana wachezaji ambao wako vizuri tangu
hapo awali kama David Silva, Sergio Aguero na Kevin De Bruyne. Hawa watatu
watakuwa ni mwanga kwa wengine watakaokuja.
“Kwa kuwa hawashiriki
kwenye michuano yoyote ya Ulaya, nadhani Chelsea watafanya vizuri kwasababu
watakuwa na muda mwingi wa kuzoeana mazoezini. Na tukumbuke kwamba ni miezi 12
tu imepita tangu wawe mabingwa, vilvile Antonio Conte ni kocha wa kiwango cha
juu.
“Nadhani Liverpool pia
watanufaika kutokana na kutokuwa na Mashindano ya Ulaya.”
Post a Comment