
ARSENE Wenger amesema kwamba
mustakabli wake ndani ya Arsenal unategemea na matokeo ya timu hiyo baada ya
msimu huu wa ligi kukamliika, lakini akasisitiza kwamba ataendelea kubaki
kwenye soka bila kujali nini kitatokea
Wenger
amebakisha mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake na Arsenal huku akiwa
ameshaitumikia klabu hiyo kwa miaka 21 sasa
Mfaransa
huyo, ambaye amesema kwamba hatafanya maamuzi yoyote kuhusu mustakabali wake
mpaka msimu ujao, alisema: “Nitakachoifanyia timu ndicho kitategemea
mustakabali wangu.”
“Huwezi
kujua. Unapaswa kufanya kazi kama ndio maisha yako ya kila siku, lakini pia
unapaswa kujua muda wowote ule unaweza kuacha,” amesema.
Wenger
amesema kwamba anaogopa sana kustaafu.
“Nitakachokifanya
ni kuendelea kufanya kazi ili mradi tu bado nina nguvu za kufanya kazi,
bila kujali ni kazi gani. Siku zote nitafanya kazi tu.”
Post a Comment