
MSHAMBULIAJI mkongwe na nahodha wa Simba SC, Mussa Hassan
Mgosi amestaafu rasmi soka na sasa anakuwa Meneja wa timu hiyo.
Mkuu
wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara amethibitisha hilo
na kusema Mgosi ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki kwa kimataifa
utakaopigwa Jumapili ya juma hili uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya URA ya
Uganda.
Manara
ameeleza kwamba aliyekuwa Meneja wa timu, Abbas Suleiman Ally anakuwa Mratibu
wa timu (Team Coordinator) kuanzia leo na nahodha mpya ni Jonas Mkude.
Aidha,
kiungo wa klabu hiyo, Peter Mwalyanzi aliyesajiliwa msimu uliopita
akitokea timu ya Mbeya City FC, ametolewa kwa mkopo African Lyon iliyopanda kucheza
ligi Kuu msimu huu wa 2016/2017.
Simba
wataingia kwenye mechi na URA wakiwapa nafasi mashabiki wao kukiona kikosi chao
kwa mara ya pili uwanja wa Taifa baada ya Agosti 8 mwaka huu siku ya Simba Day
kuichapa 4-0 AFC Leopard ya Kenya.
Inaelezwa
mechi na URA itakuwa ya mwisho ambapo Agosti 20 wataanza ligi kuu kwa
kuchuana na Ndanda FC uwanja wa Taifa.
Lakini
wakati huouo mtandao wa habari za michezo Mpenja Sports umeripoti kwamba,
mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa Taifa Stars, amekanusha taarifa za
kutunduka daruga.
MPENJA SPORTS imemtafuta Mgosi
na kumuuliza juu ya taarifa hizo na maelezo yake ni haya: “Kwanza napenda
kukanusha suala lililoandikwa kwenye mitandao la Mgosi kustaafu, Mgosi kama
Mgosi, suala la kustaafu mpira bado sana, Pogba (Paul) atakapostaafu ndipo
atafuatia Mgosi kustaafu”. Amesema Mgosi na kuongeza”
Hata
hivyo, Mgosi ameonesha wazi yuko tayari kufanya kazi yoyote ndani ya Simba hata
kama atakuwa nje ya uwanja, kitu kinachoashiria yuko mbioni kutundika daluga.
“Mimi
ni mchezaji wa Simba, ni Mfanyakazi wa Simba, nipo tayari kufanya majukumu
yoyote yanayoihusu Simba, aidha katika uchezaji au sekta nyingine.”
Mgosi
anayeheshimika ndani ya Simba amesema kutekeleza majukumu mengine nje ya kucheza
ndani ya Simba alishaanza msimu uliopita, lakini hakuna aliyehusisha na
kustaafu soka.
“Kuisaidia
Simba nje ya uwanja nimelifanya hilo toka mwaka jana, lakini mbona
halijaandikwa hivyo, mwaka jana nimekuwa msaidizi wa Mayanja (Jackson),
nilimsaidia kila kitu kama kocha msaidizi”. Amesisitiza Mgosi na kufafanua:
“Unapozungumza mtu kustaafu tuwe na subira, lazima niseme mwenyewe, sio
mitandao iandike, wengine wanaandika wapate comments, likes na kushtusha watu
ambao wananihitaji.”
MPENJA SPORTS imemuuliza kama anaamini muda wa kustaafu umefika na yuko
tayari kuwa Meneja wa Simba.
“Sio
tatizo, ni jukumu ambalo nitalifanyia kazi kwa vile ninavyofahamu mimi,
ukitaka kuangalia kiongozi anayeweza kuingoza Simba kwa kila kitu, hakuna mtu
ambaye kwa haraka unaweza kumuangalia zaidi ya Mgosi, kwasababu ni mtu
ninayeheshimika na wachezaji, naheshimika na mashabiki, naheshimika na viongozi
wa Simba, naamini katika sekta yoyote nitakayopewa Simba, hakuna atayepinga,
kwahiyo najivunia klabu yangu ya Simba,” ameongeza Mgosi.
Licha
ya kakanusha kustaafu rasmi, taarifa za ndani ambazo MPENJA SPORTS imezipata ni
kuwa kweli Mgosi anaelekea kustaafu na mechi ya Jumapili dhidi ya URA itakuwa
maalum kwake kuagwa, lakini yeye mwenyewe na uongozi hauko tayari kulizungumzia
kwasababu kuna masuala kadhaa wanajadiliana.
Inaelezwa
keshokutwa Jumamosi, Mgosi atakutana na viongozi wa Simba kujadili suala la
nafasi wanayotaka kumpa ikiwemo kuandaa mkataba .
Post a Comment