SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: WILLIAMS AJIUNGA NA EVERTON
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya klabu ya Everton kumruhusu beki wao tegemezi John Stones kujiunga na klabu ya Mancity, timu hiyo yenye makazi yake huko Mersey...

Baada ya klabu ya Everton kumruhusu beki wao tegemezi John Stones kujiunga na klabu ya Mancity, timu hiyo yenye makazi yake huko Merseyside imekamilisha dili la usajili wa beki wa klabu ya Swansea City Ashley Williams kwa kitita kinachosemekana kuwa ni pauni 12mil

Williams, 31, anakuwa mchezaji wa tatu kununuliwa na kocha mpya wa klabu hiyo Ronaid Koeman, baada ya kuwachukua Idrissa Gueye mchezaji kiungo wa Senegal na golikipa Maarten Stekelenburg. 

Lakini pia klabu hiyo ya Everton bado wapo kwenye mazungumzo na kiungo wa klabu ya Crystal Palace, Yannick Bolasie na beki wa klabu ya Sunderland, Lamine Kone.

"Ninaamini klabu inakwenda kwenye uelekeo sahihi," Alisema Williams.

Beki huyo ambae amesaini kandarasi ya miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo  amesema alikuwa anawaza siku moja kufanya kazi na kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi Koeman.
"Amekuwa ni moja ya watu wenye uwezo wa kuwaunganisha wachezaji kwa pamoja, hivyo nikitazamacho sasa mbeleni ni kujifunza vingi chini yake” Williams aliuambia mtandao rasmi wa klabu hiyo.

Awali klabu ya Swansea ilikataa ofa ya pauni 10mil kutoka Evertona na sasa wamepokea pauni 12mil baada ya kumuuza mchezaji wao tegemezi kwa matajiri wa jiji la Manchester, klabu ya Manchester City kwa pauni 47mil.

Williams alikuwa moja ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Wales kilichotolewa katika hatua ya nusu fainali ya mataifa ya ulaya na timu ya taifa ya Ureno, lakini pia Williams hakucheza mechi yeyote ya kirafiki kutokana kuwa na likizi ndefu baada ya mashindano ya EURO ya Ufaransa.

Williams ameichezea Swansea City kwa takribani miaka 8 tangu ajiunge nao mwezi march  kwa pauni 300,000 akitokea klabu Stockport na kucheza mechi 300.

Mbali na raia wa Ivory Coast Kone 23, anayefukuziwa na klabu hiyo, lakini pia wamesema wangependa kuendelea kuw na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Lukaku licha ya klabu yake ya zamani ya Chelsea ikionekana kutaka kumrudisha.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top