RAIA wa Ethiopia Almaz Ayana
ameishindia Afrika dhahabu ya kwanza Michezo ya Olimpiki mjini Rio na kuvunja
rekodi ya dunia mbio za mita 10000 wanawake.
Ayana aliwaacha nyuma wapinzani wake mbio zikiwa katikati na
kuendelea hadi mwisho, muda wake ukiwa dakika 29 sekunde 17.45.
Rekodi ya awali ilikuwa 29:31.78 na iliwekwa na Mchina Wang
Junxia mwaka 1993. Mkenya Vivian Cheruiyot ameshinda fedha naye raia mwingine
wa Ethiopia Tirunesh Dibaba akachukua shaba.
Post a Comment