SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MO BEJAIA WASEMA WAKO TAYARI KUIVAA YANGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WAPINZANI wa timu Yanga, klabu ya FC MO Bejaia ya nchini Algeria leo imefanya mazoezi katika uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam...

WAPINZANI wa timu Yanga, klabu ya FC MO Bejaia ya nchini Algeria leo imefanya mazoezi katika uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Africa.

Mchezo huo utafanyika siku ya kesho, majira ya kuanzia saa kumi za jioni kwa majira ya Africa mashariki ukiwa ni mchezo wa tano kwa timu zote mbili.

Wenyeji, klabu ya Yanga wanaingia kwenye mchezo huo, wakiwa wanaburuza mkia katika msimamo wa kundi A wakiwa na point poja pekee baada ya kucheza michezo minne na kukubali kufungwa michezo itatu, huku wakitoka sare ya mchezo mmoja dhidi ya klabu ya Medeama ya nchini Ghana.


Klabu ya MO Bejaia wao wanaingia kwenye mchezo huo, wakiwa wa tatu kwenye msimamo wa kundi hilo baada ya kukubali kufungwa mechi moja huku wakitoka sare mechi mbili na kushinda mechi moja.

Kwa upande wa Yanga, kupitia kwa kocha msaidizi wa klaabu hiyo, Juma Mwambusi, alipokuwa anaongea na msemaji wa TFF Alfrd Lucas, amesema, Yanga imejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo, japo kuna baadhi ya wachezaji wao muhimu.

“Sisi tupo vizuri, tumejiandaa vizuri kabisa japo tutawakosa wachezaji wetu muhimu kama vile Donald Ngoma yeye ana kadi mbili za njano na Mwashiuya ambae ana maradhi ya muda mrefu” Mwambusi Alisema.


Kwa jedwali la kundi A linasomeka hivi.

Timu…                                  MP    W     D      L      G       PNTS   
1.       MAZEMBE                           4       3       1      0      5:1       10
2.       MEDEAMA                           4       1       2      1      5:5        5
3.       MO BEJAIA                          4       1       2      1      1:1        5
4.       YOUNG AFRICAN              4       0       1      3       2:6        1



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top