JUMATANO: Tetesi za usajili ulaya.

Swansea wanataka kupanda dau kumsajili Leonardo Ulloa, 29,
kutoka Leicester, wakati wakijiandaa kwa kuondoka kwa Andre Ayew na Bafetimbi
Gomis (Daily Telegraph), mshambuliaji wa Wales Hal Robson-Kanu ambaye ni
mchezaji huru amepewa mshahara wa pauni 100,000 kujiunga na Ligi Kuu ya China
(Daily Mirror). Beki wa England John Stones, 22, ameiambia klabu yake ya
Everton kuwa anataka kujiunga na Manchester City (Liverpool Echo).

Chelsea wana wasiwasi kuwa huenda wakalazimika kulipa zaidi
ya pauni milioni 50 kumsajili beki Kalidou Koulibaly, 25, kutoka Napoli
(Evening Standard), Real Madrid wameingia kwenye mbio za kumsajili kiungo wa
Valencia Andre Gomes anayefuatiliwa na Chelsea (Fichajes), Madrid wameamua
kutomuuza mshambuliaji wao, Alvaro Morata, 23, kwenda Chelsea (Daily Mail
Mshambuliaji Wilfried Bony, 27, anajiandaa kuondoka
Manchester City, huku Galatasaray wakitoa pauni milioni 3 za kumsajili kwa
mkopo (Sun), Leroy Sane, 20 anayesakwa na Manchester City, hajaiambia klabu
yake ya Schalke kuwa anataka kuondoka, wakati meneja mpya wa City Pep Guardiola
akiwa tayari kutoa pauni milioni 40 kumsajili kiungo huyo Mjerumani (Daily
Star).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari
kumsajili kiungo kutoka Spain, Cesc Fabregas, 29, ambaye alikuwa naye Chelsea
(Daily Mirror), Mourinho huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Newcastle, Moussa
Sissoko, 26, iwapo atashindwa kumsajili Paul Pogba kutoka Juventus (Le 10
Sport), Man United wanaendelea kumfuatilia beki wa West Ham, Reece Oxford, 17
(Evening Standard), meneja msaidizi wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs,
41, atacheza katika ligi kuu ya India mwezi huu (Daily Mail)
Meneja wa Sunderland Sam Allardyce anaonekana huenda akatajwa
kuwa meneja wa England na Gary Neville kuwa msaidizi wake (Daily Mirror), dau
la pauni milioni 25 la Arsenal kumtaka beki Daniele Rugani, 21, limekataliwa na
Juventus (Calciomercato), Arsenal wako tayari kuwapa Napoli Olivier Giroud, 29,
pamoja na pauni milioni 42, ili wamsajili Gonzalo Higuain, 28 (Sun), Arsenal na
Chelsea wanamfuatilia beki wa Roma Kostas Manolas, 25 (Corriere Dello Sport).
Liverpool na Tottenham hawajakatishwa tamaa na bei ya pauni
milioni 25 iliyowekwa kwa beki wa Kols, Jonas Hectors, 26 (Bild), Middlesbrough
waliopanda daraja wanataka kumsajili beki wa Chelsea Tomas Kalas, 23 (Daily
Express), Middlebrough pia wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Valencia
Alvaro Negredo, 30, aliyeichezea Manchester City kwa misimu miwili (Guardian).
Wawakilishi wa Moussa Sissoko wamemtaka meneja wa Newcastle,
Rfael Benitez, kuingilia kati mzozo kuhusu bei ya pauni milioni 35 aliyowekewa
kiungo huyo ambayo wanahisi inamzuia kuondoka (Daily Mirror), Newcastle wako
tayari kusikiliza dau la kuanzia pauni milioni 20 kumsajili Sissoko, 26, ambaye
aling’ara kwenye michuano ya Euro 2016 (Times), Marseille wataelekeza nguvu zao
kumtaka Carlos Sanchez, 30, baada ya kushindwa kumpata Idrissa Gana kutoka
Aston Villa (Birmingham Mail).
Post a Comment