AZAM MEDIA yamwaga mabilioni kwa vilabu VPL
Kampuni ya kurusha matangazo ya
televisheni, AZAM MEDIA wameshinda tenda iliyokuwa imetangazwa na shirikisho la
mpira wa miguu TFF ya kituo kitakachoweza kurusha matangazo ya mechi
zinazochezwa live kwenye ligi ya VPL.
Mkataba mpya wa Azam Media kurusha
matangazo Live ya Ligi Kuu Bara utagharimu Sh bilioni 23.
Mkataba wa awali, kila klabu ilikuwa
inapata Sh milioni 100 kwa msimu lakini sasa itaingiza karibu mara mbili ya
hizo.
Katika mkataba uliosainiwa leo,
klabu itapata Sh milioni 42 kwa mafungu matatu ambayo ni Sh milioni 126.
Fungu la mwisho la milioni 42
litatolewa kwa mfumo tofauti ambao utakuwa hivi.
Timu inayoshika nafasi ya juu katika
msimamo itkuwa inafaidika kwa kupata zaidi na itakwenda hivyo hadi chini.
Maana yake ligi itakapoisha, timu zitakazokuwa
juu kimsimamo zitapata fedha nyingi zaidi na zilizo chini zitaendelea kusota
kwa kupata kiduchu.
Lengo kuu ni kuhakikisha kunakuwa na
ushindani wa kila kikosi kuona umuhimu wa kukaa juu katika msimamo wa ligi hali
itakayochangia ushindani uwanjani kwa kila timu kutaka kushinda karibu kila
mechi ili mwisho wa ligi ifaidike.
Post a Comment