SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Sababu zaainishwa, Kufukuzwa kwa Kiiza Msimbazi
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katibu Mkuu wa klabu ya Simba SC Patrick Kahemele amekiambia kituo kimoja cha radio cha jijini Dar es Salaam kwamba, kutemwa kwa m...

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/11/Hamisi-Kiiza-Diego.jpg



Katibu Mkuu wa klabu ya Simba SC Patrick Kahemele amekiambia kituo kimoja cha radio cha jijini Dar es Salaam kwamba, kutemwa kwa mshambuliaji raia wa Uganda Hamisi Kiiza kumetokana na nidhamu yake mbovu ndani ya klabu hiyo.
Kahemele amesema kamati ya usajili ya Simba imeamua kuachana na mshambuliaji huyo baada ya kukaa nae mara kadhaa lakini hakukuwa na mabadiliko ndipo walipoamua kuchukua uamuzi wa kuachana naye.
“Mchezaji akianza kuleta maneno maneno au akianza kufanya vurugu inakuwa shida na inaweza kuharibu timu nzima. Na mwaka huu Simba imepania kufanya vizuri kwahiyo haiwezi kuruhusu virusi ndani ya klabu,” aesema Kahemele ambaye ameanza kutekeleza majukumu yake kama Katibu Mkuu wa Simba tangu Julai mosi alipotambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari.
Kiiza aliifungia Simba magoli 19 magoli mawili nyuma ya Amis Tambwe mfungaji bora wa msimu uliomalizika na kuisaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL nyuma ya Azam FC na mabingwa wa ligi hiyo Yanga SC.

 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top