SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: JUMANNE: Tetesi za usajili barani Ulaya.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
JUMANNE: Tetesi za usajili barani   Ulaya.   Chama cha soka cha England, FA, kitazungumza na meneja wa Hull City Steve Bruce, wakati...

JUMANNE: Tetesi za usajili barani  Ulaya.

 Steve Bruce

Chama cha soka cha England, FA, kitazungumza na meneja wa Hull City Steve Bruce, wakati wakiendelea na harakati za kutafuta meneja mpya wa England (Daily Telegraph), uhamisho wa Graziano Pelle kutoka Southampton kwenda Shandong Luneng ya China kunamfanya mshambuliaji huyo 30 kuwa mchezaji wa sita anayelipwa zaidi duniani akipata pauni 260,000 kwa wiki (Sun).

 

               

 

 

 

 

 

 

 

 

 Viungo Juan Mata 28 na Bastian Schweinsteiger 31 pamoja na mabeki Marcos Rojo na Daley Blind 26 wanaonekana kama wachezaji wa ziada katika mipango ya meneja mpya wa Manchester United, Jose Mourinho (Daily Record), Villareal nao wamejiunga na Everton katika mbio za kumwania kiungo Juan Mata wa United (Daily Express).

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsajili beki wa Atletico Madrid, Lucas Hernandez, 20, kwa pauni milioni 20 (Sun), mshambuliaji kutoka Colombia, Marlon Moreno, 19, atasaini mkataba wa miaka mitano kwenda Man City, lakini atakwenda Deportivo La Coruna kwa mkopo msimu ujao (Daily Mirror), mwenyekiti wa West Ham, David Gill amesema klabu yake haitosikiliza dau lolote chini ya pauni milioni 50 kumtaka kiungo kutoka Ufaransa, Dimitri Payet 29 (BBC Radio 5).

 Sam Allardyce set for England interview

Lazio wako tayari kumwacha Filipe Anderson 23 kuondoka, huku Chelsea wakimtaka kiungo huyo (Gazzetta World), Chelsea pia wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona, Arda Turan 29 ambaye pia ananyatiwa na Arsenal (Sport), Chelsea vilevile wanajiandaa kutoa pauni milioni 34 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon, Joao Mario 23 (A Bola).

 Lucas Hernandez

Liverpool wamejitoa katika kutaka kumsajili kiungo wa Bayern Munich Mario Gotze 24, huku Tottenham na Borussia Dortmund wakiendelea kumtaka (Liverpool Echo), kipa wa zamani wa Arsenal, Alex Manninger, 39, anafanya mazoezi na Liverpool akiwa na matumaini ya kupata mkataba (Sun), beki Martin Skirtel 31 anatarajiwa kuwasili Istanbul kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 5.5 kutoka Liverpool kwenda Fernabahce (Daily Mirror).

Everton wamepanda dau la pauni milioni 25.5 kumtaka beki wa Juventus Daniel Rugani 21 (Calcio Mercato), Christian Benteke 25 hakaribii kuondoka Liverpool na kwenda Crystal Palace, kwa mujibu wa wakala wake (Evening Standard), Inter Milan wameweka bei ya pauni milioni 43, kwa klabu inayomtaka mshambuliaji wake Mauro Icardi, 23, ambaye anasakwa pia na Tottenham (AS), Newcastle watafikiria kumuuza kiungo Moussa Sissoko, 26, kwa timu itakayokuwa tayari kulipa pauni milioni 35 (Independent

 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top