SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Kikosi bora cha Euro 2016.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi bora cha Euro 2016.   Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo, anayechezea Real Madrid ya Uhispania, ni miongon...


Kikosi bora cha Euro 2016.
 
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo, anayechezea Real Madrid ya Uhispania, ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kwenye kikosi bora cha michuano ya Euro 2016 kilichotangazwa na Shirikisho la Soka Ulaya, Uefa.
Ronaldo aliwahi kujumuishwa katika kikosi cha mashindano ya ulaya mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19 lakini pia na mwaka 2012.
Raia mwenzake, Pepe pia yupo kwenye kikosi hicho na aliwahi pia kujumuishwa 2008 na 2012.
Awali, kulikuwa kukitajwa kikosi cha wachezaji 23 lakini wakati huu kimetajwa kikosi cha wachezaji 11
Kikosi kamili kinajumuisha (4-2-3-1): Rui Patrício (Ureno); Joshua Kimmich (Ujerumani), Jérôme Boateng (Ujerumani), Pepe (Ureno), Raphaël Guerreiro (Ureno); Toni Kroos (Ujerumani), Joe Allen (Wales); Antoine Griezmann (Ufaransa), Aaron Ramsey (Wales), Dimitri Payet (Ufaransa); Cristiano Ronaldo (Ureno).
Kikosi hicho kiliteuliwa na jopo la kiufundi cha Uefa lililojumuisha, miongoni mwa wengine, Sir Alex Ferguson na David Moyes.
“Tunaamini kikosi hiki cha wachezaji 11 kinawakilisha wachezaji bora zaidi walioshiriki michuano,” amesema, Ferguson, ambaye ni balozi mwema wa ukufunzi wa Uefa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top