West Ham: Yamnasa Gokhan Tore Kutoka klabu ya Besiktas kwa Mkopo.

West Ham
wamefanikiwa kumsajili winga machachari kutoka klabu ya Besiktas kwa mkopo,
akitia kandarasi ya mwaka mmoja huku kukiwa na uhuru wa kumsajili jumla endapo
atakuwa na msimu bora klabuni hapo.
Tore raia wa
Ujerumani aliyezaliwa nchini Uturuki, ameichezea timu ya vijana ya Chelsea kwa
miaka miwili kabla ya kuihama klabu hiyo na kusajiliwa na Besiktas
Tore
aliisaidia klabu yake kuichapa klabu ya Fenerbahce na kuchukua ligi ya
Uturuki.
Tore mwenye umri wa miaka 24 amesema, Bilic alikuwa ni sababu ya yeye kuhama uwanja wa Olympic na kuongeza kuwa alikuwa ni meneja bora kwa wakati wote nikiwa naye.

Post a Comment