SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle: ajiunga na timu ya Shandong Luneng ya Nchini China.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle: ajiunga na timu ya Shandong Luneng ya Nchini China. Mshambuliaji wa kimataifa wa iI...
Mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle: ajiunga na timu ya Shandong Luneng ya Nchini China.
Graziano Pelle




Mshambuliaji wa kimataifa wa iItalia aliyekuwa akikipiga katika klabu ya Southampton ya nchini Uingereza, amejiunga na klabu ya Shandong Luneng inayoshiriki  super league ya nchini China kwa uhamisho wa paund 12m.
Pelle mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na ligi ya EPL msimu wa 2014 akitokea katika klabu ya Feyenoord ya nchini Uholanzi  na kuishindia Sants magoli 30 katika mechi 81 alizocheza Pelle.
Pelle aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa akiwa anaichezea klabu ya Southampton na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki katika mashindano ya EURO yaliyomalizika hapo siku ya jana na kuifungia timu yake ya taifa magoli mawili.
Pelle anakuwa mchezaji wa tatu kuihama klabu ya Southampton baada ya kushuhudia raia wa Kenya Victor Wanyama kusajiliwa na klanu ya Tottenham lakini pia Sadio Mane akijiunga na majogoo wa anfield, klabu ya Liverpool.


Pelle aliyewahi kuzichezea klabu za Parma pamoja na AZ Alkmaar, amejiunga na aliyowahi kuwa mchezaji wa zamani wa New castle Papiss Cisse ambao kwa sasa wako chini ya kocha aliyewahi kuifundisha klabu ya Fulham ya nchini Wingereza Felix Magath.
Klabu ya Southampton wanakaribia kuinasa saini ya mchezaji kiungo mkabaji wa Bayern Munich Pierre-Emile Hojbjerg ambaye anafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kutangazwa rasmi kwa kitita cha paund 12.8m.

 




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top