
Mchezaji wa klabu ya Liverpool na timu ya tai fa ya England,
James Milner ameamua kutundika daruga kucheza sokam la kimataifa.
James Milner, 30, aliyewahi kucheza klabu ya Manchester City
amecheza michezo 61 tangu ajumuishwe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England
mwaka 2009.
Milner amecheza fainali mbili za kombe la dunia, 2010 na 2014
na fainali za mataifa ya ulaya mbili za mwaka 2012 na za mwaka huu ambapo
nahati mbaya alicheza dakika tatu pekee katika fainali za mwaka huu za nchini
Ufaransa.
‘‘Kufanya maamuzi ya kustaafu soka la kimataifa ni akili ya
kawaida sana, Kikubwa, niwatakie mafanikio, Sam Allardyse, Big Sam, kocha mpywa
wa timu ya taifa ya England, wachezaji, uongozi, pamoja na mashabiki wote wa
timu ya taifa ya England” Alisema Milner.
Milner alishinda goli moja pekee wakati England iliposhinda
goli 5-0 dhidi ya timu ya taifa ya Moldova, hatua ya kufuzu fainali za kombe la
dunia mwaka 2014 likiwa ni goli pekee katika kariya yake kwenye timu ya taifa.
Post a Comment