
Klabu ya wekundu wa
msimbazi Simba imehamisha kambi yake toka mjini Morogoro hadi jijini Dar es
salaam katika hoteli ya Dege Beach kwa ajili ya kuendelea kujiandaa na siku ya
Simba day itakayofanyika siku ya jumatatu tarehe nane ya mwezi huu ambapo
wataadhimisha miaka 80 ya klabu hiyo.
Wakiwa Morogoro, Klabu ya
Simba ilifanikiwa kucheza mechi nne za kirafiki ambapo walifanikiwa kushinda
mechi tatu na kupoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya klabu ya KMC.
Klabu hiyo iliyo chini ya
mwlimu Joseph Omog, raia wa Cameroon itajitupa uwanjani kucheza dhidi ya klabu
ya Leopords ya nchini Kenya mchezo ambao wangecheza na klabu ya Zimbabwe japo
klabu hiyo ya Inyerclube ikajitoa mapema.
Post a Comment