SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: HALI ILIVYOKUWA BAADA YA MANJI KUTANGAZA KUJIUZULU.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
BAADA  ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kutangaza kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti pamoja na kusitisha zoezi lake la kuikodi klabu ya Y...
Mashabi-Yanga

BAADA ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kutangaza kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti pamoja na kusitisha zoezi lake la kuikodi klabu ya Yanga, Mashabiki na wanachama wa Yanga wamekusanyika kwenye ofisi za klabu hiyo wakipinga kujiuzulu kwa Manji.
Baadhi ya wanachama na mashabiki wamekuwa wakidai kwamba kuna watu ambao hawataki kumuunga mkono Manji katika zoezi zima la kutaka kuikodi timu pamoja na nembo kwa miaka 10.
Aidha, moja ya watu ambao wamekuwa wakitajwa kukwamisha zoezi hilo ni mzee Akilimali, pamoja na watu wengine wanaopinga kusudi la mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji kuikodi klabu hiyo.

Manji amefikia maamuzi hayo baada ya kusema kwamba amekuwa akitukanwa sana na baadhi ya watu ambao hawataki Manji kuimiliki klabu hiyo ya Jangwani, “Hela za kwangu mwenyewe, kwanini nikukanwe sasa? Basi waje wenjewe” Manji alisema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top