
Wachezaji hao
waliwasili Dar Alhamisi na wakafanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
Yanga itaikaribisha
Medeama kwa mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya makundi katika uwanja wa
taifa Dar es Salaam.
Mchezao huo utaanza
saa 10.00 jioni
Michezo miwili ya
awali ya Yanga katika michuano hiyo ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria
ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi
iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Wakati
wapinzani wao Medeama wana pointi mija pekee baada ya kupoteza mchezo wao dhidi
ya TP mazembe ya nchini Congo wakati wakiambuliapointi moja walipotoka sare ya
bila kufungana na klabu ya Algeria ya Bejaia, mchezo uliofanyika nchini Ghana.
Mchezo wa Jumamosi
utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din atakayekuwa
mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi
wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid Mansour, kwa mujibu wa Shirikisho la
Kandanda la Tanzania (TFF).
Post a Comment