Jana usiku Juni 14,
nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Ally Samatta alifunga
goli kwenye mchezo wa hatua za awali kuwania kucheza Europa Ligue wakati Genk
ikicheza dhidi ya Buducnost Podgorica.
Mchezo
huo ulimalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 huku Samatta akiwa
amefunga bao la pili dakika ya 79 huku baada ya Neeskens Kebano kufunga
bao la kwanza dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati.
Huu ni mchezo wa raundi ya
pili ya michuano ya UROPA na mchezo wa marudiano utafanyika tarehe 21 ya mwezi was
saba.
Post a Comment