SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: KLOPP AMEFUNGUKA JUU YA MATUMIZI YA PESA NYINGI KWENYE USAJILI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesisitiza kwamba yeye si muumini wa matumizi makubwa ya fedha linapokuja suala la usajili wa wachezaji ...
Generated by  IJG JPEG Library
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesisitiza kwamba yeye si muumini wa matumizi makubwa ya fedha linapokuja suala la usajili wa wachezaji na kusema kwamba kutumia mil 100 kwa ajili ya kununua mchezaji ni njia sahihi ya kuendesha soka.
Mjerumani huyo ameongeza wachezaji Sadio Mane na Georginio Wijnaldum, lakini uhamisho wa wachezaji hao hauwezi kufananisha na ule wa paundi mil 100 unaoripotiwa kufanywa na Manchester United kwaajili ya kunasa saini ya Paul Pogba kutoka Juventus.
Hata hivyo, Klopp amesema kwamba hana mpango wa kufanya usahihi wa aina hiyo, na kueleza wasiwasi wake juu ya hasara inayoweza kupatikana kutokana na kiwango hicho cha fedha.
“Kama unanunua mchezaji mmoja kwa paundi mil 100 na halafu anapata majeraha, hapo ndipo utakapoona hasara yake.”
“Kikubwa ninachopenda mimi ni kuhakikisha najenga timu imara yenye wachezaji wenye umoja na kufanikiwa kwa pamoja.
“Timu nyingine zinaweza kwenda kutafuta wachezaji wa gharama kubwa. Nataka niwe tofauti kidogo, lakini pia ningefanya tofauti hata kama ningekuwa na kiasi hicho cha fedha.
“Sijui ni kiasi gani cha fedha ambacho tungeweza kutumia kwasababu hakuna aliyeniambia, hapana huwezi kufanya hivi’.
“Kama natumia pesa, ni kwasababu najaribu kujenga timu, timu halisi. Barcelona walifanya hivyo. Unaweza kushinda ubingwa, unaweza kushinda mataji, lakini kuna jinsi ambavyo unahitaji kushinda.”
Klopp amesema kwamba hana mpango wowote wa kushinda na vilabu vingine katika kuwania wachezaji.
Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amesema angependa zaidi kuangalia umuhimu wa mchezaji ambaye anaweza kuwa na faida kwa timu yake.
Klopp amesema: “Kama wote mnaogelea kwenye bwawa moja, basi lazima litakuwa dogo – na hatimaye hamuwezi kutosha, sasa ndivyo ilivyo kwenye uwanaiaji wa wachezaji.
“Kuna wachezaji wengi tu nje ya bwawa, wachezaji wazuri kwa hatima ya baadaye. Tunajitahidi kadri tuwezavyo kuwapata.
“Mchezaji mzuri wa msimu uliopita ni vizuri kumfahamu lakini inavutia zaidi kujaribu kutafuta mchezaji ambaye siku za usoni anataraji kuwa mchezaji bora.
“Kama unaweza kufanya hivyo sasa, unaweza kuwa usajili rahisi kuliko wote. Na hivyo ndivyo tunavyojitahidi kufanya.
“Ni suala tu la kuwa mbunifu, kwasababu ubunifu ni jambo zuri sana. Ni suala la kutafuta wachezaji ambao wanaweza kwenda pamoja na sisi.”


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top