
Kiungo wa Manchester
United Bastian Schweinsteiger ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa
baada ya kucheza michezo 120 kwa taifa lake la Ujerumani.
Schweinsteiger (31) ni moja ya wachezaji waliocheza mechi
nyingi zaidi kwa taifa lake, huku akiwa amecheza michezo mitano tu kwenye Euro
mwaka huu na kufanikiwa kufika mpaka nusu fainali, ambapo walitolewa na
Ufaransa.
Schweinsteiger, ambaye kwa mara kwanza kabisa alicheza
Ujerumani mwaka 2004, amefanikiwa kuwemo kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la
Dunia mwaka 2014 baada ya kuifunga Argentina, baada ya kumaliza katika nafasi
ya tatu mwaka 2006 na mwaka 2010. Vile vile ana medali ya shaba aliyopata
kwenye michuano ya Euro mwaka 2008.
“Muda si mrefu, nimemwomba kocha asinijumuishe tena
kwenye kikosi cha timu ya taifa kwenye siku zijazo, kwasababu ninataka
kustaafu,” aliandika
“Nimefanikiwa kucheza michezo 120 kwa taifa langu na
nimepata wasaa mzuri sana ambao hakika nashindwa hata jinsi ya kuelezea na kwa
maana ya uzuri na mafanikio pia.”
“Joachim Low alijua namna gani ya Michuano ya Euro ya mwaka
huu iliyofanyika nchini Ufaransa ilivyokuwa na maana kwangu kwasababu kiukweli
nilitaka kushinda taji ambalo hatujaweza kulipata tangu tulivyofanya hivyo
mwaka 1996.
“Lakini ndiyo hivyo tena haikuwa bahati yangu, lazima
nikubaliane na hali halisi.
“Kushinda Kombe la Dunia mwaka 2014 ilikuwa ni jambo la
kihistoria ya aina yake ambayo kiukweli siwezi hata kuelezea.
“Na ndiyo maana ni sahihi na inaleta maana kuchukua
maamuzi haya na kuitakia timu mafanikio mema katika harakati za kufuzu kucheza
Kombe la Dunia mwaka 2018.
“Nimeamua kuchukua maamuzi ya kuacha kuitumikia timu ya
taifa ambayo imekuwa familia bora sana kwangu. Natumaini kwamba mahusiano yangu
hayatavunjika bali yatabaki kuwa imara kwa namna moja ama nyingine.
“Mimi ningependa tu kuwaambia mashabiki wetu: ‘ilikuwa ni
heshima kubwa sana kucheza kwaajili yenu ninyi. Shukrani nyingi sana nielekeze
kwenu na asanteni sana kwa kila kitu ambacho tulifanya bega kwa bega.”
Post a Comment