
Mashabiki wa klabu ya
Wekundu wa Msimbazi Simba wamekusanyika makao makuu ya klabu hiyo maeneo ya
Kariakoo mtaa wa Msimbazi wakishinikiza timu ikabidhiwe kwa MO DEWJI huku
viongozi wa klabu hiyo wakiwa hawataki kufanya zoezi hilo.
Hapo jana mfanyabiashara
huyo alikuwa na mkutano na waandishi wa habari akitaja vipaumbele vilivyomfanya
Dewji kutaka kuinunua klabu hiyo huku swala kubwa likiwa ni kama mshabiki
mkereketwa lakini akisisitiza ya kuwa hana maana ya kuinunua klabu hiyo kwa nia
ya kumuingizia hela kwani tayari yeye alishakuwa na vyanzo si chini ya 100
ambavyo vinamuingizia kipato chake, hivyo anaitaka hisa ya asilimia 51 ya klabu
hiyo.
Uongozi wa klabu hiyo
tayari umepanga kuwa na mkutano wa wanachama utakaofanyika hapo kesho ikiwa ni
juu ya kutaka kumwachia timu MO na kujadili mambo mengine kadha wa kadha haswa
swala la Simba day litakalofanyika siku ya tarehe 8 ya mwezi ujao huku
wakuazimisha miaka 80 ya kuanzishwa kwa klabu hiyo.
Post a Comment