
MASHINDANO ya AFCON yanayoendelea huko nchini Gabon, yamezidi
kushika kasi baada ya kushuhudia leo mchezo mmoja ukipigwa.
Baada ya hapo jana kutawala kwa sare mbili zimwi hilo
limeendeleea tena leo kwa mchezo wa awali ambapo Mbweha wa jangwani, timu ya
taifa ya Algeria ililazimisha sare baada ya kutoka 2-2 dhidi ya timu ya taifa
ya Zimbabwe.
Magoli ya Algeria yamefungwa na mshambuliaji wa klabu ya
Leicester, Riyad Mahrez wakati magoli ya Zimbabwe yamewekwa kimiani na Kudakwashe Mahachi na Nyasha Mushekwi.
Kwa matokeo haya yanafanya mpaka sasa
kutokuwepo kwa timu yeyote ambayo imeandikisha ushindi baada ya hapo jana
wenyeji kubanwa mbavu na Guinea Bisau wakati Burki na Faso wakiwabana mbavu
Cameroon.
Mchezo
unaotarajia kuanza hivi punde ni kati ya Senegal watakaowavaa Mali.
Post a Comment