
BAADA
ya kuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga kila mechi, kocha wa klabu ya Tottenham
Spurs Mauricio Pochetino amemwambia Delle Alli aendelee kuwa mwiba awapo ndani
ya box la wapinzani.
Wakiwa
wanajiandaa kuwakabili West Brom katika dimba la white hart Lane, Pochettino
amemsisitizia Delle kuwa na mwendelezo wa makali yake ili wazidi kuwanyemelea
wale walio kileleni mwa ligi hiyo.
Delle
amefanikiwa kupachika mabao 7 ndani ya mechi 4 alizoanza na kuwavutia mabosi wa
vilabu vya Hispania kutaka kupata kandarasi yake.
Post a Comment