SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MOURINHO ALIITIA HASARA CHELSEA BAADA YA KUTIMULIWA 2015
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KUFUKUZWA kwa aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, kama mkufunzi wa Chelsea, kumeiingizia klabu gharama ya £8.3m ikiw...
Jose Mourinho


KUFUKUZWA kwa aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, kama mkufunzi wa Chelsea, kumeiingizia klabu gharama ya £8.3m ikiwa ni kama fidia.

Mourinho, ambaye ni kocha wa Manchester United, alitimuliwa mwezi December ya mwaka 2015 kufuatia matokeo mabuvu ya kushindwa kulitetea kombe la ligi.

Chelsea, walimaliza msimu wakiwa nafasi ya 10 ya msimamo wa EPL na taarifa ya mapato ya mwaka 2015-2016 inaonyesha klabu ilipata hasara ya Zaidi ya £70.6m ikijumuishwa na £67m iliyolipwa kwenye kampuni ya Adidas kusitisha mkataba.

 Hata hivyo, mkataba wa Adidas ulivunjwa ili kuingia kandarasi na kampuni ya Nike kwa Zaidi ya miaka 15 ambapo wataweza kutengeneza faida ya £30m kwa mwaka.


Mkataba wa Adidas na Chelsea ambao ulikatishwa ndani ya miaka 6 ulikuwa umesainiwa kwa jumla ya miaka 10 ambapo ungeiingizia Chelsea kiasi cha £30m kwa mwaka.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top