SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: PAYET AWAVURUGA MABOSI WA WEST HAM UNITED.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KOCHA wa timu ya West Ham, Slaven Bilic amethibitisha ya kuwa mshambuliaji wao tegemezi, Dimitri Payet amegoma kusaini mkata wa ku...


Dimitri Payet celebrates scoring the second goal for West Ham with manager Slaven Bilic

KOCHA wa timu ya West Ham, Slaven Bilic amethibitisha ya kuwa mshambuliaji wao tegemezi, Dimitri Payet amegoma kusaini mkata wa kuendelea kubaki klabuni hapo.

Kufuatia taarifa hiyo, Bilic ameamua kumtoa kwenye kikosi kitakachocheza na Crystal Palace siku ya jumamosi.

Payet alikuwa na msimu bora sana uliopita na kuisaidia timu kupata matokeo chanya hivyo anataka kuondoka klabuni hapo ili akatafute maisha sehemu nyingine.

“Ndio hili lipo kwamba Payet anataka kuondoka, hataki kufanya mazoezi na timu na tulishasema hatutawauza wachezaji wetu bora kama Payet” Alisema Bilic.

Mabingwa wa ligi ua Ufaransa, klabu ya PSG wanahusishwa kutaka kumsajili Payet raia wa Ufaransa ambaye ameshapachika mabao 15 ndani ya mechi 60 alizocheza.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top