
NI jambo jepesi sana
kuiendeleza rekodi kuliko kuivunja na hicho ndicho Simba walichokifanya baada
ya kuwagaraza klabu ya Yanga na kuwaachia kidonda baada ya kuwaondosha kwenye
mapinduzi Cup kwa jumla ya penalt 4-2.
Mchezo huo ulioshuhudia
timu hizo zikitoshana nguvu kwa dakika zote 90, ambapo mwamuzi wa mchezo huo
aliamuru kupigwa matuta yaliyopeleka maumivu mitaa ya Jangwani.
Penati za simba zilipigwa na Jonas Mkude, Daniel Agyei, Mzamiru Yassin na Javier
Boukungu huku Method Mwanjale akiwa ni mchezaji pekee wa Simba aliyekosa penati
ambayo iliokolewa na golikipa wa Yanga Deogratius Munishi.
Simon
Msuva na Thaban Kamusoko ndio wachezaji pekee wa Yanga waliofunga penati zao
huku Deogratius Minish ‘Dida’ na Mwinyi Haji penati zao zilitua kwenye mikono
ya golikipa wa Simba Daniel Agyei.
Mashindano
hayo yanatarajia kufikia tamati siku ya Ijumaa ambapo maadhimisho ya siku
yenyewe ya Mapinduzi ni siku ya Alhamisi.
Post a Comment