SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Historia fupi Ya MAZEMBE.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
                                                       MAZEMBE HISTOR NA charles kunji Ilikuwa ni mwaka 1939 kitika mji wa ...

                                                       MAZEMBE HISTOR




NA charles kunji
Ilikuwa ni mwaka 1939 kitika mji wa elizabethvile ambao kwa sasa ukifahamika kama Lubumbashi, mmisionari mmoja akifahamika kwa jina la  Benedictine aliyekuwa akiiongoza taasisi ya saint Boniface yaani mtakatifu Boniface alipamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu ikifahamika kwa jina la saint georges, Katika kikundi cha vijana wa skout kwaajili ya kutoa burudani.
Jina la la saint georges lilikuwa ni jina la patron wa kikundi cha vijana wa scout.
Tangu kuanzishwa kwa timu hiyo, mashindano yake ya kwanza saint Georges iliweza kumaliza katika nafasi ya tatu. Nyuma ya fc leopard ya prince Charles kwa sasa ikifahamika kama VIJANA KATUBA pamoja na klabu ya Lubumbashi.
Saint georges iliweza kuvuka katika vipind kadha wa kadha, na katika mwaka 1944 waliweza kubadili jina na kuitwa saint paul FC baada ya vijana wa scout kuondoka. Miaka kadhaa baadae baada ya wamisionari kushindwa kuihudumia timu hiyo, ndipo kampuni ya matairi ikachukua nafasi ya wamisionari na kuibadili timu kwa jina la ENGLEBERT.
Tangu congo ilipopata uhuru juni 30 ya mwaka 1960 mpaka miaka ya 1966, englebert iliweza kufanyiwa marekebisho  kwa kununua wachezaji wapya waliokuja kutia chachu klabuni na kuifanya klabu hiyo kuchukua makombe ikiwemo Katanga cup pamoja na CONGO CUP.
Katika miaka minne mfululizo iliyocheza englerbert katika fainali ya klabu bingwa Africa, englebert ilifanikiwa kuchukua mataji mawili kati ya manne iliyocheza kuanzaia mwaka 1967-70.
Mbali na AL AHLY YA MISRI ILIYOCHUKUA mara 8 katika ngazi ya vilabu barani Africa, LITUPISWA ENGLEBERT MAZEMBE wao wamenyanyua kwapa mara tano.
Mafanikio na changamoto ni mambo yasiyoepukika waliyopitia klabu ya englebert MAZEMBE, lakini mafanikio ni pale walipoweza kufika katika hatua ya fainali ya clabu bingwa ya dunia mwaka 2010 iliyofanyika katika mji wa abbuu dhabi  huko uarabuni walipoweza kukubali kichapo cha magoli matatu kwa sifuri toka kwa internationali milan iliyokuwa chini ya hoseph morinho.
Katika mashindano ya klabu bingwa barani Africa mwaka 2011 katika hatua ya pili ya mashindano hayo, mazembe walipangwa kukutana na klabu ya simba ya jijini dar es salaam na katika mechi zote mbili wekundu wa msimbazi simba wakaweza kulala kwa jumla ya magoli sita kwa tatu. Baada ya mechi hiyo, milango ya mbwana ally samata ikawa imefunguliwa na kupata nafasi ya kusajiliwa na klabu hiyo na kuisaidia timu hiyo kuchukua makombe kadha wa kadha lakini pia kumpelekea samata kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa wachezaji wa ligi ya Africa.
Siku ya jumanne ya wiki ijayo, Mazembe watajitupa uwanjani dhidi ya klabu ya kutoka jijini dar es salaam , wakati huu si wekundu wa msimbazi tena,  wala wa matopeni, bali ni wana manjano wa mtaa wa jangwani hawa ni young African sports clubyaani yanga wa kimataifa. Katika mchezo wa kundi A wa shirikisho barani Africa.
Sekunde na dakika vyote vinakimbia kwa speed kuelekea tarehe ishirini na nane ya mwezi wa sita saa kumi za jioni wakati mwafaka wa mechi hiyo.

Kila la kheri young African sports club kuelekea mchezo huo, mkiingia kwa tahadhari ya kuwa mnacheza na clabu kubwa duniani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top