SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Mwendelezo wa hatua ya mtoano EURO2016
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
               MATOKEO NA MECHI ZA LEO.       Na charles Kunji Michezo ya hatua ya mtoano yaani kumi na sita bora imeanza katika ...
       
       MATOKEO NA MECHI ZA LEO.
     






Na charles Kunji
Michezo ya hatua ya mtoano yaani kumi na sita bora imeanza katika viwanja tofauti ambapo kwa michezo ya jana tulishuhudia Uswisi wakaweza kutolewa nje ya michuamno ya EURO baada ya kukamilisha dakika 120 wakiwa wamefungana magoli moja kwa moja dhidi ya Poland na ndipo matuta yakaja kuamua nani wa kuendelea baada ya Poland kushinda penati zote 5 huku wapinzani wao Uswis wakiambulia penati 4 na hivyo kutupwa nje ya michuano.
Katika mchezo wa majira ya saa moja jioni Northern  Ieland wakaweza kukubali kichapo cha goli moja kwa nunge dhidi ya vijana wa Wales waliokuwa wakiongozwa na NALE pamoja na RAMSEY na hivyo kuwafanya Northern kuaga mashindano hayo.
Katika mchezo wa mwisho kwa siku ya jana uliweza kuzikutanisha timu ya Ureno waliofuzu kwa kutumia mlango wa tatu  na Croatia Viongozi wa kundi D na mchezo kwenda mpaka dakika mia na ishirini. Katika dakika 90 timu zote ziliweza kutoshana nguvu na hivyo kutoa sare tasa ya bila goli na kufanya mwamuzi wa mchezo huo kuongeza dakika 30. Mchezo wote kwa ujumla ulikuwa ni wa kushambuliana kwa zamu na wote kutokutumia nafasi walizokuwa wakizipata. Upande wa Croatia, 
Kiungo mshambuliaji wao anayekipiga katika clab ya Real madrid LUCAS MODRIC akashindwa kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi na kumpa nafasi mshambuliaji wa timu pinzani RONALDO anayekipiga timu moja na MODRIC kutengeneza nafasi ya kushinda goli na golikipa kuweza kuutema mpira mbele ya Quaresma aliyemalizia na kuifanya ureno kuibuka na ushindi wa goli moja kwa sifuri goli lililofungwa dakika za mwishoni.
Baada ya matokeo hayo, hivyo katika hatua ya robo fainali ya kwanza itazikutanisha timu ya ureno ikiongozwa na CHRISTIAN RONALDO na Polland wakiongozwa na mshambuliaji anayekipiga katika clab ya beyrn munich LEWANDOSKI. Wales watabidi kusubiri matokeo ya mechi za leo ndio wajue watakutana na nani katika hatua ya robo fainali.
Mechi za leo tarehe 26 mwezi wa sita, siku ya jumapili, wenyeji Yfaransa wakiongozwa na DIMITR PAYET watajitupa uwanjani leo saa kumi jioni kukipiga na timu ya taifa ya Ireland katika mchezo wa kutafuta timu itakayofuzu hatua ya robo fainali.
Ireland wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa na ufaransa goli la mkono katika kutafuta timu itakayocheza kombe la dunia mechi iliyofanyika mwaka 2009.
Ukiachilia mbali mechi ya ireland na ufaransa, lakini pia kutakuwa ma mechi ya ujerumani dhidi ya slovakia ambapo wakati mwaka 2010 wakati pweza alikuwa akitabiri matokeo, mwaka huu sio pweza tena bali ni Lesa [tembo] Mwenye umri wa miaka 49 yeye ametabiri ujerumani kushinda mechi hiyo.
Mechi ya mwisho kwa siku ya leo itawakutanisha timu ya Hangury watakaowavaa Ubelgiji.






About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top