SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MCHEZO WA YANGA DHIDI YA JKT RUVU KUAHIRISHWA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
picha na Bin Zubery. MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga SC na JKT Ruvu uliokuwa ufanyike Jumatano Uwanj...

picha na Bin Zubery.


MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga SC na JKT Ruvu uliokuwa ufanyike Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeahirishwa.

Habari ambazo charleskunji,blogspot.com imezipata kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimesema kwamba mchezo huo uliopangwa kuchezwa Jumatano ya Agosti 31 sasa utapangiwa tarehe nyingine.

Na hatua hyo inatokana na Yanga kuomba uahirishwe kwa sababu ina wachezaji wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Wachezaji hao ni kipa Deogratius Munishi 'Dida', mabeki Vincent Andrew 'Dante', Kelvin Yondani na Mwinyi Hajji, kiungo Juma Mahadhi na mshambuliaji Simon Msuva.

Aidha, Yanga pia imesema wachezaji wake wengine, beki Vincent Bossou (Togo), kiungo Haruna Niyonzima (Rwanda) na mshambuliaji Amissi Tambwe (Burundi) nao pia wameitwa na timu zao za taifa na kufanya idadi ya wachezaji wanane.

Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinaruhusu timu ambayo wachezaji wake wasiopungua watano wameitwa timu za taifa kuahrishiwa mechi. 

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ ameita wachezaji 20 watakaosafiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba ya mechi za Kundi G kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).

Mbali na Dida, Yondani, Dante, Mngwali, Mahadhi  na Msuva wengine ni Aishi Manula, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Shomari Kapombe (Azam FC) na David Mwantika (Azam FC).

Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Shiza Kichuya (Simba SC), Ibrahim Jeba (Mtibwa Sugar), Jonas Mkude (Simba SC), Muzamil Yassin (Simba SC), na Farid Mussa (Teneriffe ya Hispania).

Washambuliaji ni Jamal Mnyate (Simba SC), Ibrahim Hajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC) na Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top