SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: AGUERO HUENDA AKAIKOSA MANCHESTER DERBY.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MSHAMBULIAJI wa   klabu ya Manchester   City, Sergio Aguero anaweza     kufungiwa michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko beki wa...



A different angle of the incident between Aguero and Reid


MSHAMBULIAJI wa  klabu ya Manchester  City, Sergio Aguero anaweza    kufungiwa michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko beki wa wagonga nyindo wa London, klabu ya West Ham Winston Reid jana na kuwa na uwezekano wa kuukosa mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester United.

Mchezaji  huyo alimfanyia tukio hilo Reid kuelekea mwishoni mwa mchezo huo ambao City walishinda 3-1, mabao yaliyofungwa na Raheem Sterling (2) na Ferndandinho. Reid alitolewa mara moja baada ya tukio hilo na kocha wake Slaven Bilic amsema alifanya hivyo kutokana na sababu za kiufundi.

Mwamuzi wa mchezo huo Andre Marriner alikuwa karibu kabisa wakati tukio lile likitokea. Aliamuru ipigwe free-kick na imeonekana kwamba hakujua kama Aguero alifanya kitendo kile.

Lakini pamoja na yote hayo FA wanaweza kuangalia upya video na kuitolea maamuzi.
Endapo Aguero atakumbana na adhabu hiyo, basi anaweza kuukosa mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester United utakaopigwa Old Trafford Septemba 10, mchezo mwingine ukiwa dhidi ya Bournemouth kabla ya kumalizia na Swansea kwenye Kombe la EFL.

Meneja wa Man City Pep Guardiola amesema: ‘Sikuliona tukio lile, hivyo siwezi kusema chochote.’

‘Natumaini hakuna baya litakalotokea. Na kama litatokea tutakubaliana nalo na kuendana nalo. Kama tutampoteza basi ndiyo tumempoteza hivyo.’

Bosi wa West Ham Slaven Bilic pia hakuona tukio hilo na kudai kwamba uamuzi wa kumtoa Reid ulikuwa umezingatia zaidi sababu za kiufundi.

‘Sikumtoa kwasababu ya tukio lile. Nilifanya vile kwasababu nilitaka kufanya madabiliko tangu awali,’ Bilic alisema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top