RAIS wa zamani wa shirikisho la mpira wa
miguu duniani FIFA Sepp Blatter, anawasilisha rufaa yake ya mwisho mahakamahi
hii leo dhidi ya marufuku aliyowekewa ya michezo na michezo kwa kukiuka madili.
Bw
Blatter anahudhuria mahakamani kusikiliza kesi hiyo inayoendeshwa na mahakama
ya usuluhishi wa mizozo michezoni nchini Uswizi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Lausanne, amejielezea kama mtu mwenye matumaini.
Bw
Blatter aliwekewa marufuku hiyo mwezi Disemba mwaka jana kwasababu aliidhinisha
malipo ya zaidi ya dola milioni mbili kwa mkuu wa zamani wa soka barani Ulaya ,
Michel Platini, miaka mitano iliyopita.
Mwezi
Mei, Bw Platini alishindwa kushawishi kuondolewa kwa marufuku dhidi yake,
ingawa ilipunguzwa kutoka miaka sita hadi miaka minne.
Post a Comment