
SHIRIKISHO la mpira barani Africa, CUF, limeweka
hadharani ratiba ya michezo ya nusu fainali ya kombe la klabu bibgwa barani
Africa pamoja na zile za shirikisho.
Kwa
upande wa Ligi ya Mabingwa, ambapo bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa
kujizolea kitita cha dola za Kimarekani Milioni 1.5 pamoja na kupata tiketi ya
kucheza Klabu Bingwa ya Dunia, Mabingwa wa zamani Zamalek ya Misri ambao
wamechukua kombe hilo mara tano watamenyana na vigogo wa Morocco, Wydad
Casablanca kuwania kutinga fainali.
Ikumbukwe
kuwa Zamalek watakuwa na ari kubwa kutokana na kuikosa hatua hii kwa takriban
miaka 10, baada ya mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 2005.
Kwa
upande wa klabu ya Zesco United ya Zambia, ambao ni mara yake ya pili kufika
hatua hii, itakuwa na kibarua kizito kumenyana na klabu ya Africa Kusini,
Mamelod Sundowns, timu ambao kwenye michuano ya mwaka huu imeonyesha upinzani
mkali sana.
Kwa
upande wa mechi za shirikisho, TP Mazembe itamenyana na Etoile du Sahel ya
Tunisia, huku MO Bejaia ya Algeria wataumana uso kwa uso na waarabu wenzao wa
FUS Rabat ya Morocco.
Klabu Bingwa
Sept 16-18, 2016
Zamalek (Misri) Vs Wydad Athletic Club (Morocco)
Zesco (Zambia) Vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
Zamalek (Misri) Vs Wydad Athletic Club (Morocco)
Zesco (Zambia) Vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
Kombe la Shirikisho
Sept 23-25, 2016
TP Mazembe (DRC) Vs Etoile du Sahel (Tunisia)
MO Bejaia (Algeria) Vs FUS Rabat (Morocco)
TP Mazembe (DRC) Vs Etoile du Sahel (Tunisia)
MO Bejaia (Algeria) Vs FUS Rabat (Morocco)
Post a Comment