Timu ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys
inatarajiwa kuondoka alfajiri ya kesho kuelekea nchini Madagasca kuweza kuweka
kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Africa ya Kusini wa fainali za kombe la
mataifa ya Africa chini ya 17 zitakayofanyika mwakani huko nchini Madagascar.
Serengeti Boys imefuzu kucheza na timu ya taifa ya vijana ya
Africa Ya Kusini baada ya kuwabugiza magoli 9-0 timu ya taifa ya vijana ya Mauritius
na hivyo kusonga mbele na kukutana na timu ya Africa ya Kusini mchezo wa kwanza
ukipigwa huko nchini Africa Ya Kusini na kuja kumalizia hapa nyumbani.
Bingwa mtetezi wa mashindano hayo, ni timu ya Mali
iliyoifunga timu ya taifa ya Africa ya Kusini kwa jumla ya goli 2-0 katika
fainali zilizofanyika nchini Gabon mwaka jana, na mwaka ujayo mwemyeji wa
mashindano haya ni Madagasca sehemu ambako Tanzania inakwenda kuweka kambi yake
kabla ya kuwavaa timu ya Africa Kusini tarehe 5 ya mwezi agosti kabla ya wao
kusafiri kuja jijini Dar es salaam.
Mbali na vijana wa Tanzania kuendelea kuisaka nafasi hiyo kwa
udi na uvumba, lakini pia, fainali za mwaka 2019 zitafanyika katika ardhi ya
nyumbani kwa hiyo Serengeti boys wakifuzu fainali za mwaka kesho, watakuwa na nafasi
nzuri, kwani watakuwa wamepata uzoefu wa kutoka ambapo mashindano yatakuwa
katika ardhi ya nyumbani.
Kila la kheri timu yetu ya Tanzania katika maandalizi
kuelekea mchezo huyo utakaopigwa tarehe 5 ya mwezi ujao.
Post a Comment