
Klabu
ya Manchester Vity imekamilisha dili la kumsajili aliyekuwa mchezaji wa klabu
ya Shakle kwa kitita cha pauni mil 37. Sane, aliisaidia Ujerumani kutinga nusu
fainali ya mchuano ya Euro 2016, aliifunga klabu yake ya Schalke mabao 33
katika ligi kuu ya Ujerumani. Schalke ilimaliza msimu katika nafasi ya 5.
''Ukimtizama
akicheza unavutiwa na ueledi wake, yaani hababaishwi na mpira wala hasuisui
hata anapopewa mpira katika mazingira magumu'' alisema Guardiola.
''Hivi unavyomuona ana
umri wa miaka 20 tu lakini tayari ameshajishindia nafasi katika timu ya taifa, hiyo
inatudhihirishia kuwa anakipaji kinachohitaji kunolewa kisha anawiri
kitaaluma''
Kwa upande wake Sane
amesema kuwa moja ya sababu kuu yake ya kujiunga na Man City ni kupata nafasi
ya kujifua chini ya ukufunzi wake Guardiola.
‘‘Wakati huu katika
taaluma yangu hii bila shaka Guardiola ndiye kocha ambaye ninahakika atanifaa
zaidi na kunikuza'' alisema Sane. ''Sitarajii kupewa nafasi moja kwa moja ila
najua baada ya muda nitapata nafasi''
Post a Comment