
JORGE COSTA amechaguliwa tena kuwa kocha wa timu ya taifa ya Gabon kwa miezi sita.
Costa 44, raia wa Ureno, awali
alichaguliwa kuwa kocha mwaka 2014, lakini mkataba wake ulimalizika tarehe 30
ya mwezi juni, na Gabon walishaanza kuandaa kuongeza nae mkataba mwingine.
Costa amekuwa akisuka mipango ya fainali
za kombe la mataifa ya Africa ambazo zitafanyika nchini humo mwaka kesho.
‘‘Ni mkataba wa malengo ya wazi na ukiwa
kama msingi wa timu yetu ya taifa kuhakikisha inafanya vyema katika ardhi ya
nyumbani” Alisema mwenyekiti wa shirikisho la mpira nchini humo.
Lakini pia wakaongeza ya kuwa sababu
zingine nje ya uwanja zitawekwa sawa ili kuhakikisha wanampa mwalimu mazingira
sawia ya yeye kufanya kazi ili aipe mafanikio timu yao ya taifa.
Costa aliyewahi kuwa beki wa timu ya
taifa ya Ureno, amefundisha timu anuwai katika nchi yake lakini pia hata nje ya
taifa lake kama vile Cyprus na Romania.
Katika kibarua chake cha awali akiiongoza
timu ya taifa ya Gabon, walitolewa katika hatua za awali ya kufuzu kombe la
dunia baada ya kushinda mechi moja na kufungwa mechi mbili katika kundi lake.
Mara ya kwanza Gabon kufuzu kombe la
dunia ilikuwa ni mwaka 1974 lakini wakashindwa kufuzu tena mpaka mwaka 1994.
Mafanikio yao makubwa ilikuwa ni mwaka
1996 walipofika hatua ya roba fainali na mwaka 2012 walipokuwa wenyeji,
wakishirikiana na Equatorial Guiena.
Post a Comment