SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MAJERAHA YAMWEKA WAWRINKA NJE YA OLYMPIC.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mcheza tenisi namba nne duniani, Stan Wawrinka raia wa Uswis, amejiengua katika mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza ijumaa hii k...

Stan Wawrinka


Mcheza tenisi namba nne duniani, Stan Wawrinka raia wa Uswis, amejiengua katika mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza ijumaa hii kwa sababu ya majeraha aliyoyapata.

Wawrinka, 31, amepatikana na majeraha katika mashindano ya Rogers Cup na hivyo kufanya mchezaji aliye ndani ya top ten ya viwango vya tenisi duniani kutokushiriki katika mashindano ya Olympic. Roger Federer, Tomas Berdych, Milos Raonic na Dominic Thiem nao pia wamejiengua katika mashindano hayo.

‘‘Nilitaka kushuhudia na kushiriki kwa mara ya tatu sasa, lakini ndo haiwezekani tena” Alisema Wawrinka. Kuumia kwa Wawrinka ni pigo baada ya mcheza tenisi nambari tatu ulimwenguni na mshindi wa medali ya shaba mwaka 2012 aliyejitoa baada ya maumivu ya goti.

Na kwa minajiri hiyo, wanabaki wachezaji wawili ambao ni Martina Hings ambae kwa mara ya mwisho kucheza ilikuwa ni mwaka 1996, na Timea Bacsinszky.

Mcheza tenisi nambari saba Milos Raioni na mcheza tenisi nambari nane  Berdych wote walijitoa kwa hofu ya virusi vya zika.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top