
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya leo wenyeji, ya Madagascar mjini Antananarivo leo.
Katika mchezo huo wa marudiano baina ya timu hizo baada ya juzi kutoka sare ya bila kufungana, mechi ya pili imemalizika kwa Serengeti Boys kupata ushindi wa goli 2-0, mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Cyprian Mtesingwa dakika 77 na Kelvin Nashon dakika ya 86.
Serengeti Boys ilikuwa imeweka kambi mjini Antananarivo, Madagascar tangu wiki iliyopita kujiandaa na mechi dhidi ya Afrika Kusini kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili wiki hii na kesho inaondoka vijana wa Serengeti Boys wanatarajiwa kuondoka kuelekea Afrika kusini.
Serengeti Boys inakwenda Afrika Kusini tayari kwa mchezo wa kwanza Jumapili, kabla ya timu hizo kurudiana Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, Chamanzi, Dar es Salaam.
Mshindi kati ya Africa Kusini na Tanznia itamenyana na mshindi wa mechi ya Congo watakaokipiga na Namibia.
Post a Comment