
Klabu ya soka ya Swansea City imekataa
dau la pauni milioni 10 lilitolewa na klabu ya Everton ili kuweza kumsajili
beki Ashley Williams.
Taarifa kutoka uongozi wa klabu hiyo zinasema, beki huyo raia wa
Wales ambae pia ni nahodha wa Swansea alikua anakaribia kufika makubaliano ya
mwisho kwenda Goodison Park kujiunga na Everton.
Williams ambae atafikisha miaka 32 mwezi huu anamkataba na timu
yake unaomalizika mwaka 2018, msemaji wa klabu hiyo anasema hawako tayari
kumuuza beki huyo.
Beki huyo ameichezea timu yake zaidi ya michezo 300 alisajiliwa
kwa kiasi cha pauni 300,000 toka klabu ya Stockport mwaka 2008.
Everton wanasaka saini ya beki huyo ili kwenda kuziba pengo
litakaloachwa na mlinzi wao mahiri John Stones anayehusishwa kutaka kujiunga na
matajiri wa jiji la Manxhester, klabu ya Manchester City.
Post a Comment