SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: CHRIS SUTTON, ''MZEE WENGER AKIFUKUZWA, THE GUNNERS WATAPATA MAFANIKIO"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na Celtic Chris Sutton ameendelea kumkandia kocha wa klabu ya Arsenal kwa kusema kwamba kamwe ...
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na Celtic Chris Sutton ameendelea kumkandia kocha wa klabu ya Arsenal kwa kusema kwamba kamwe Klabu hiyo isitarajie ubingwa kama timu hiyo itaendelea kuwa chini ya ya mkufunzi huyo. Katika dirisha hili la usajili Arsenal wamemsajili Granit Xhaka tu, huku wenzao Manchester City, Manchester United na Chelsea wakiwa wamefanya usajili wa maana kuimarisha vikosi vyao kwaajili ya msimu mpya.
Sutton ambaye alibeba kombe la Ligi ya England akiwa na Blackburn Rovers, amemlaumu Arsene Wenger kwa kutoonesha nia ya dhati ya kufanya usajili wa kusiaidia timu na kusisitiza Mfaransa huyo anahitaji kuachia ngazi kwa manufaa ya timu.
“Nina mashaka makubwa na Arsenal katika msimu huu tena. Hawajaonesha nia yoyote mpaka sasa,”Sutton aliiambia BBC Five.
“Nadhani bodi na Wenger wanawaangusha sana mashabiki wao. Mimi sijui ni wapi Arsenal wanaelekea, kama ningekuwa ni shabiki wa Arsenal, basi ningehuzunika sana.
“Wamesema hawatatumia fedha nyingi, bodi inafurahia tu jambo hili, au uongo? Kila mwaka, wao kazi yao ni kushiriki Ligi ya Mabingwa na kupata fedha.
“Wenger sio kocha mwenye malengo na Arsenal tena, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda taji msimu uliopita, lakini alishindwa. Hawataki kutumia pesa, na kama wewe ni shabiki wa Arsenal, jitathmini vizuri, maana kila mwaka itakuwa ni mwendo wa ‘top four’ tu.
Halafu unaona timu kama Manchester United, Manchester City wanaonesha nia ya ubingwa msimu huu, hili linazidi kuleta ugumu zaidi kwa Arsenal, nasema hivi….mpaka Wenger aondoke ndipo Arsenal watatwaa ubingwa.”

Hayo ni maneno ya Sutton akionyesha waziwazi kumkandia kocha Arsene Wenger kwa kusema kwamba, kuendelea kuwepo kwake klabuni hapo, ndiyo sababu ya klabu hiyo kutokutwaa mataji. Kumbe Sutton anamaanisha mafanikio ya klabu hiyo ni siku wamemwacha mkufunzi huyo raia wa Ufaransa na kumsajili kocha mwingine, ndiyo watapata mafanikio.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top