SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MABINGWA WA EPL WAKUBALI TENA KIPIGO KINGINE.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mchezo wa kirafiki kati ya mabingwa wa ligi kuu nchini Hispania FC BARCELONA na mabingwa wa ligi  kuu nchini England, klabu ya Leiceste...

Mchezo wa kirafiki kati ya mabingwa wa ligi kuu nchini Hispania FC BARCELONA na mabingwa wa ligi  kuu nchini England, klabu ya Leicester city, the Fox, umemalizika kwa mabingwa wa EPL kukubali kipigo cha magoli 4-2
Alikuwa ni Munir katika dakika ya 26 alipokwamisha mpira wavuni na kuiandikia klabu ya Barca goli la kuongoza huku magoli mengine yakifungwa na Suarez dakika ya 34, na Munir kurudi tena nyavuni dakika ya 45 na kufanya mpaka mapumziko Leicester wakiwa nyuma kwa goli 3-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa the fox kufanya mabadiliko na kuwaingiza baadhi ya wachezaji wao wapya kama vile Ahmed Mussa, pamoja na Mendy na dakika ya 48 Mussa akawanyanyua mashabiki wa Leicester kwa kuiandikia timu yake goli la kwanza.
Wakati, mbweha hao wakihaha kutafuta magoli ya kusawazisha, Mshambuliaji wao aliyesajiliwa toka CSKA MOSCOW ya Urusi akapachika bao la pili dakika ya 67 na kurudisha nguvu ya kuweza kusawazisha magoli yote.
Rafael Mujica, ndiye aliyekata matumaini ya Mbweha hao baada ya kuipatia timu yake goli la nne mnamo dakika ya 84 na mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho, ubao ulikuwa unasomeka kama Barca 4-2 Leic.
Mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki takribani 42,879, ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Leicester kucheza na mabingwa wa ligi mbalimbali, wa kwanza ukiwa ni dhidi ya timu ya PSG ambapo pia napo walikubali kipigo cha mbwa mwizi cha magoli 4-0.

Baada ya mchezo huo, mkufunzi wa klabu ya Leicester, Claudio Ranieri akasifu sana uwezo wa Mussa aliyemsajili toka CSKA Moscow na kusema atafanya makubwa akiwa klabuni hapo.

‘‘Nimefurahishwa sana na Mchezaji Mussa, ni jambo la muhimu sana kwa kikosi kama chetu kuwa na mchezaji mwenye maamuzi ya haraka sana na ameonyesha uwezo wake” Alisema Ranieri.

Leicester city watakuwa na mechi wikiendi hii na klabu ya Manchester United mechi ya ngao ya hisani kabla ya ligi kuu kuanza rasmi tarehe 13 ya mwezi huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top