
Beki wa kati wa klabu ya
Barcelona, Martin Montoya, amejiunga na klabu ya Valencia kwa dili la miaka
minne baada ya kuruhusiwa na klabu yake huku vilabu vyote vikiwa vimekubaliana
kwa pamoja hapo jana.
Montoya 25, raia wa
Hispania alipandishwa katika timu ya wakubwa mwka 2011 lakini akashindwa
kuonyesha uwezo wake katika mechi zote 45 alizocheza na hivyo kusababisha
maisha yake Camp Nou kuendelea kuwa magumu.
Klabu ya Valencia na
Montoya mwenyewe wamekwishafikia makubalianoo na hivyo Montoya atasaini
kandarasi ya miaka minne kuihudumu klabu hiyo ya Valencia inayoshiriki ligi kuu
ya Hispania.
Montoya ametumia muda
wake mwingi akiwa klabu ya Inter kwa mkopo pamoja na Real Betis msimu uliopita
na anatarajiwa kukiimarisha kikosi cha Valencia akiwa kama sehemu ya kikosi
hicho.
Post a Comment