
Klabu ya Southampton imemsajili golikipa
Alex McCarthy kwa mkataba wa miaka mitatu toka timu ya Crystal Palace.
McCarthy, alicheza michezo saba msimu uliopita akiwa na klabu yake ya Crystal
Palace huu ni usajili wa tatu wa klabu hiyo ya Southampton baada ya kuwasajili
Nathan Redmond Pierre-Emile Hojbjerg.

Wakati huo, beki Steven Taylor amejiunga na timu ya
Portland Timbers, inayoshiriki ligi ya kuu ya Marekani akitokea Newcastle
United. Beki huyo amekaa kwenye klabu ya Newcastle kwa muda wa 21 toka akiwa
mdogo, na amecheza michezo 268.

Post a Comment