
Kocha wa Chelsea Antonio Conte hana hakika juu ya majaliwa ya mshambuliaji Diego Costa, wakati vyombo vya habari nchini Uhispania vikiripoti kuwa mshambuliaji huyo huenda akarejea katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
Kamba ya Costa raia wa
Hispania kwa kocha mpya wa klabu ya Chelsea ni kama hapewi nafasi kubwa
kuendelea kuwapo kwenye kikosi cha Chelsea na ndio maana waandishi wengi wa
habari wamekuwa wanaripoti juu ya urejeaji wake kwenye klanu yake ya zamani ya
Atletico Madrid.
Lakini pia hata uongozi
wa klabu ya Atletico, umeonesha nia ya kutaka kumrudisha mshambuliaji wao ili
aweze kujumuika nao huku mshambuliaji mwingine raia wa Hispania Torres akiwa
anahusishwa na kuihama klabu hiyo.
Post a Comment