Mkufunzi wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amesema Alex
Oxlade-Chamberlain atakuwa na msimu bora baada ya kuwa na msimu mredu wa majeraha
uliomuweka nje ya michuano ya EURO2016.
Oxlade-Chamberlain 22, alishinda goli wakati klabu yake ya
Arsenal iliposhinda goli 3-1 dhidi y0000a Chivas
de Guadalajara huko nchini Marekani, katika michezo ya kirafiki.
Chuba Akpom pamoja na Rob Holding, aliyejiunga
na Arsenal mwezi Julai, pia walishinda katika mchezo huo.
Mkufunzi wa washika mitutu wa London, Wenger
amesema, anaamini Oxlade Chamberlain
atakuwa na msimu bora pale ligi itakapokuwa imeanza rasmi na atatoa mchango
mkubwa kwenye kikosi chake.
Oxlade-Chamberlain amekuwa nje kwa muda mrefu
nah ii yote imekuwa inasababishwa na majeraha ya mara kwa mara lakini tangu
arsenal wamekuwa na michezo ya kirafiki, Chamberlain amekuwa ni sehemu ya
kikosi cha Arsene Wenger.
Post a Comment