
Klabu ya Real Madrid, imesema haina matarajio ya haraka ya kufanya faida ya mchezaji wao Alvaro Morata, baada ya mabingwa hao wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE kuamua kumrudisha mchezaji huyo toka klabu ya Juventus mwezi uliopita.
Morata aliuzwa klabu ya Juve misimu miwili iliyopita huku akisaini mkataba wa kurudishwa tena kama atafanya vyema na kuiwezesha klabu ya Juve kushinda magoli 27 katika mechi 93 alizocheza lakini pia kuishindia timu yake ya taifa magoli matatu kwenye michuano ya ulaya.
Ripoti ya vyombo vya habari nchini Uhispania na England zimependekeza kuwa huenda Zidane akamrudisha na kudumu klabuni hapo kwa siku kadhaa baada ya klabu za nchini England kuonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo, taarifa ambayo imekanushwa vilivyo na zidane na kusema ya kuwa Morata alikuwa sehemu ya mipango yake.
''Ndio, Morata ni mchezaji wa Real Madrid" Zidane aliwaambia waandishi wa habari huko Michgan baada ya ushindi wake wa 3-2 dhidi ya klabu ya Chelsea wikiendi iliyopita.
''Tuna furaha ya kuwa amerudi tena Bernabeu sehemu alipokulia Morata na sasa amekuwa mchezaji wetu na tutakuwa nae kwa muda mrefu" Alieleza Zinedine Zidane.
Post a Comment